Tuesday, February 26, 2013
Waraka wa Tatu wa Lema Kwa Rais Kikwete
Mh Rais Nakusalimu .
Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma .
Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma .
Saturday, February 23, 2013
DEMU MPYA WA DIAMOND WAMFANANISHA NA WEMA.
Avril Nyambura.
IMEBAINIKA kuwa, mwanamuziki ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na
Nasibu Abdul ‘Platnumz’, Avril Nyambura ni staa anayetingisha kwa
skendo nchini Kenya lakini anapendwa ile mbaya.
Chanzo cha habari ambacho kinaishi nchini Kenya kililiambia Ijumaa hivi
karibuni kuwa, Avril kwa skendo anatisha lakini cha ajabu ni staa wa
kike anayewavutia wengi nchini humo.
“Yaani Avril ni kama Wema wa Kenya, anatisha kwa skendo, kila siku magazeti yanamuandika na hivi karibuni aliandamwa na ishu ya usagaji, cha ajabu anapendwa sana. Yaani ni kama ilivyo kwa Wema wa Tanzania,” alisema mdau huyo.
“Yaani Avril ni kama Wema wa Kenya, anatisha kwa skendo, kila siku magazeti yanamuandika na hivi karibuni aliandamwa na ishu ya usagaji, cha ajabu anapendwa sana. Yaani ni kama ilivyo kwa Wema wa Tanzania,” alisema mdau huyo.
MNYIKA VS NAPE, FORM FOUR RESULTS NAPE NNAUYE
MNYIKA VS NAPE, FORM FOUR RESULTS
NAPE NNAUYE
DIV IV-29
KISW D, HIST D, GEOG D, ENG F, B/MATH F, BIOL D, CHEM D, PHY D, CIV
JOHN MNYIKA
DIV I-7
PHY A, CHEM A, BIOL A, CIV A, ENGL A, GEOG A, HIST A, B/MATH A, KISW A, B/KNOW A
MY TAKE: MNYIKA NI GINIAZI
NAPE AJIENDELEZE
Ref; Jay Chadema
— with Chadema Bunda and 44 others.
MNYIKA VS NAPE, FORM FOUR RESULTS
NAPE NNAUYE
DIV IV-29
KISW D, HIST D, GEOG D, ENG F, B/MATH F, BIOL D, CHEM D, PHY D, CIV
JOHN MNYIKA
DIV I-7
PHY A, CHEM A, BIOL A, CIV A, ENGL A, GEOG A, HIST A, B/MATH A, KISW A, B/KNOW A
MY TAKE: MNYIKA NI GINIAZI
NAPE AJIENDELEZE
Ref; Jay Chadema
— with Chadema Bunda and 44 others.NAPE NNAUYE
DIV IV-29
KISW D, HIST D, GEOG D, ENG F, B/MATH F, BIOL D, CHEM D, PHY D, CIV
JOHN MNYIKA
DIV I-7
PHY A, CHEM A, BIOL A, CIV A, ENGL A, GEOG A, HIST A, B/MATH A, KISW A, B/KNOW A
MY TAKE: MNYIKA NI GINIAZI
NAPE AJIENDELEZE
Ref; Jay Chadema
Patrice Muamba uanjani tena
Yule mchezaji mahiri aliekua akikiputa kwenye timu ya bolton Wanderers alielazimishwa kustaafu baada ya kuangua kuanjani kwa tatito la moyo kusimama kwa muda wa masaa 78.
Jumapili hii atakua katika uanja wa taifa wembley akikabizi kombe kwa mshindi wa kombe la ligi
Friday, February 22, 2013
BEKI BLACK STARS (John Paintsil) AMEMSHAMBULIA MKEWE NA KUMJERUHI VIBAYA
Mlinzi wa Black stars(Ghana) amekamatwa na yupo chini ya pilice kwa kosa la kumjerui mkewe.
Taarifa hili imetolewa na kituo cha police cha mjini Accra, Greater Accra Police PRO Freeman Tettey kwenye intaview aliofanya na Joy News Muda mfupi uliopita.
Ilikiri kua ukweli bado haujajulikana ila sababu zilizopelekea kufanya hivyo na kutoelewana kati ya John na mkewe.
Taarifa ya mwandishi Haruna Maiga alioko maeneo ya Legon police ambopo John Paintsil ameshikiliwa anasema kua John aliletwa police hapo akiwa na watoto wake watatu akiwa na kundi la police kama escot ya kumfikisha kituo cha police
Katika taarifa ya mwanzo katika jalada la police linasemakana John ameandikiwa makosa mawili kua amefanya shambulio na kutoa lugha chafu ya matusi kwa mkewe.
Mkewe, Richlove Paintsil aliruka ukuta wa nyuma yao na kuingia kwa nyumba ya jirani kujinusuru na ugomvi uliokua ukirindima ndani ya nyumba yao dhidi yake na mumewe John.
Richlove amejeruhiwa vibaya maeneo ya jicho na mumewe.
Ugomvi wote huo ulisababishwa na skendo zilizokua zikivuma kuhusu John kua alikua anatoka nje ya kambi kipindi cha kombe AFCON 2013 nnchi africa ya kusini kuwaletea wenzake wanawake wakustarehe nao ambayo ilipekea Black Stars kufanya vibaya
katika mashindano hayo skata hilo lilianzishwa na shabiki mmoja ambae pia ni mtangazaji wa redio Nnchi humo
Kanisa katoliki laruhusu tembe za kuzuia mimba
Kanisa Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.
Tembe za kuzuia mimba
Uamuzi huu umefanywa kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.
JCB Afunga Ndoa...
Rapper kutoka kundi la Watengwa lililopo A-City, JCB ambae hivi karibuni ametoka kuachia track yake inayokwenda kwa jina la Niende Wapi akiwa ameshirikiana na Domokaya amevuta jiko hivi karibuni...
JCB sasa ameuacha u-bachelor rasmi baada ya kufunga ndoa rasmi siku ya jumatano ya Tarehe 20 mwezi huu. Ndoa hii imeonekana kuwa ni ya kimya kimya sana maana sio watu wengi waliokuwa wakijua juu ya tukio hilo.
Hizi ni baadhi ya picha za kwenye harusi hiyo...
Diamond Platnumz Azungumzia Kuhusu Mganga Aliyejitokeza...
Hivi karibuni, alijitokeza mganga wa kienyeji akidai kumfanyia Diamond Platnumz dawa za kienyeji za ziada ili aweze kuwa na nyota nzuri kwenye muziki na kung'ara kama alivyo sasa.
Mganga huyo alikwenda katika moja ya magazeti ya udaku ya hapa nchini na kudai, Platnumz amekuwa hapokei simu zake hasa baada ya kufanikiwa katika muziki na maisha yake kiujumla huku haikuwa hivyo kipindi cha mwanzo.
Diamond alikuwa kimya na muda mrefu na mara kwa mara amekuwa akikanusha habari hizi kuwa si za kweli na kusema hamjui mganga huyo na kuwa yeye hashiriki vitu kama hivyo.
Lakini hivi karibuni Diamond ameamua kuongea ukweli hasa pale alipofanya interview a kituo kimoja cha Redio cha hapa jijini Dar na kuzungumza almost kila kitu kuhusu suala hili.
Msikilize Mr. Diamonds akiongea hapa chini:
Bofya Hapa
Wanafunzi wajiua kwa matokeo kidato cha IV
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Rutta
Matokeo
mabaya ya mtihani wa taifa wa kumaliza kidato cha nne wa mwaka 2012
yamesababisha maafa baada ya wahitimu wawili waliofeli kujinyonga.
Wahitimu waliojinyonga katika matukio mawili tofauti ni wa mikoa ya Tabora na Dar es Salaam.
Katika tukio la kwanza, mhitimu katika Shule ya Sekondari ya Kanyenye
mjini Tabora ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mwinyi Kata ya Chemchem,
Manispaa ya Tabora, Michael Fidelis (19), amejinyonga.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Tabora, Anthony Rutta, alisema mwanafuzi huyo alikwenda kuangalia
matokeo Jumatatu saa 11:00 jioni huu na baadaye alikutwa amejinyonga
hadi kufa chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila.
Kamanda Rutta alieleza kuwa marehemu alipata daraja la sifuri na kwamba
aliacha ujumbe uliosomeka: “Nisamehe sana mama usitafute mchawi,
nakupenda sana, uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo mabaya,
nakutakia maisha mema.”
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kenyenye, Kapufi Patson, alisema kuwa
mwanafunzi huyo alikuwa ni mpole na mtaratibu na wameshangazwa na uamuzi
aliouchukua wa kujinyonga.
Matokeo ya shule hiyo yanaonyesha hakuna mwanafuzi aliyepata daraja la
kwanza wala la pili isipokuwa waliopata daraja la tatu ni wawili, la nne
ni 14 na waliopata sifuri ni 85. Wahitimu 36 matokeo yao yameuiliwa kwa
sababu ya kudaiwa ada ya mtihani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo
ALIYEJINYONGA DAR
Katika tukio la pili, mhitimu katika Shule ya Sekondari Debrabant
iliyopo Mbagala, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Barnabas Venant
(18), amejinyonga kutokana na matokeo mabaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema jana kuwa
kijana huyo, mkazi wa Nzasa, alikutwa amejinyonga kwa kamba aina ya
manila ndani ya stoo ya nyumba yao.
Kamanda Kiondo alisema, tukio hilo lilitokea juzi saa 10:00 jioni baada
ya kijana huyo kutoridhishwa na matokeo ya mtihani huo ambayo alipata
daraja la nne, tofauti na matarajio yake.
Alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke.
HAKIELIMU YAKOSOA
Wakati huo huo, serikali imelaumiwa kuwa ndiyo chanzo cha matokeo mabaya
ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana, kutokana na
kutotumia tafiti na mapendekezo mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na
asasi mbalimbali na wataalamu.
Aidha, imepewa angalizo kuwa wanafunzi watakachaguliwa kujiunga na
kidato cha tano, wawe ni wale waliofaulu bila ya kutumia kigezo cha
kuchagua hata wanafunzi waliopata daraja la nne kwa nia ya kujaza nafasi
za kidato cha tano kama ilivyofanya kwa waliojiunga na kidato cha
kwanza mwaka 2013.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Elizabeth Missokia,
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu kupitia tamko kwa vyombo vya habari
kuhusiana na matokeo ya kidato cha nne.
Missokia alisema HakiElimu walianza kuitahadharisha serikali na jamii
kuhusiana na hali mbaya tangu mwaka 2010, baada ya asilimia 49 ya
wanafunzi waliofanya mtihani kidato cha nne kupata daraja sifuri.
“Tulitoa angalizo kuwa kama juhudi za makusudi kuboresha ufundishaji na
ujifunzaji hazitafanyika, basi tutarajie idadi kubwa ya wanafunzi kufeli
miaka ijayo na ndicho kimetokea kwani tumeanza kuvuna tulichopanda,”
alisema.
Missokia aliwaasa wananchi kuhakikisha kwamba serikali haiendelei
kubahatisha katika suala la utoaji wa elimu kwa kuwa wana wajibu wa
kuishinikiza kwenye suala la utoaji wa elimu bora kwa watoto wa
Kitanzania kwa mustakabali wa taifa.
Akizungumzia watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, Missokia
alisema kwa kuangalia matokeo ni dhahiri kwamba wanafunzi takribani
23,520 kati ya 367,750 waliofanya mtihani, ndiyo wanaostahili kujiunga
na kidato hicho.
Alisema wanafunzi hao 23,520 wamepata kati ya daraja la kwanza na la tatu ambayo ni asilimia sita tu ya waliofanya mtihani.
“Serikali isirudie kuchukua hata wale ambao hawakufaulu kama ilivyokuwa
kwa waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, ilipoamua kuchukua
wanafunzi wenye alama chini ya 100 kati ya 250, uamuzi ulioonyesha
dhahiri kukosa msimamo,” alisema.
Aliitaka serikali kutambua kuwa viwango vya udhahili kwa ngazi yoyote
ile ya elimu hasa ufaulu, vina mantiki ya pekee kumuwezesha mwanafunzi
kumudu masomo katika ngazi anayodahiliwa.
Alisema kitendo cha kuendelea kudahili wanafunzi ambao hawana sifa ni
kuendelea kupeleka wanafunzi ngazi za juu za elimu, wakati hawana uwezo
wa kuyamudu masomo katika ngazi hiyo.
Pia alisema HakiElimu imeshangazwa na sababu zilizotolewa na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, kuwa ukosefu wa walimu
na maabara ulichangia wanafunzi wengi kufeli.
Missokia alisema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2009, ikama ya walimu
sekondari ilikuwa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 50 hadi 55, na kwamba
ikama ya sasa ni ya mwalimu mmoja kwa wanafunzi kati ya 35-38, hali
inayoonyesha kuvuka kiwango kinachotakiwa cha mwalimu mmoja kwa
wanafunzi 40.
“Pia shule nyingi hazikuwa na maabara wakati huo kuliko sasa, lakini
wanafunzi waliofeli sasa wamezidi kuongezeka na kufikia asilimia
takribani 61. Kwa hiyo hali hii haihitaji majibu au sababu nyepesi
alizozitaja waziri,” alisema.
Alitaka kuwapo mjadala wa kina kwa wananchi na wabunge kuishikiza
serikali kutambua kuwa mfumo wetu hauko sawa na kubainisha changamoto za
kuurekebisha haraka kupunguza athari zitakazolikumba taifa hili na
mustakabali wa elimu.
CHANZO: NIPASHE
Mchungaji Antony Lusekelo azungumzia Kuchinja!
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa
hivi.
Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.
Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.
Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".
Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.
Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.
Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.
Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.
Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".
Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.
Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.
HATIMAE WIZ KHALIFA NA AMBA ROSE WAPATA MWANA
ILIKUA HIVI KWENYE MITANDAO KIBAO YA KIJAMII
Wiz Khalifa and Amber Rose Welcome Their First Child
IKIFWATIWA NA BO BO BONGEE LA PIC YA JAMAA AKIWA PANDE ZILEE
Haikuishi hapo, kitu kihapen kama jamaa amechangamka nane kwenye twitter pale alipotupia kama hivo hapo chini "Daddy Time" Then akatupia mpaka jina ....
endelea
"Happy Birthday Sebastian "The Bash" Taylor Thomaz!!! ?????? Everyone welcome this perfect young man into the world"
Wiz Khalifa (@wizkhalifa
Kama vipi endelea kucheki twitter account yake ujionee mwenyewe
https://twit ter.com/wizkh alifa/status/ 3047145605632 08192
Nae Amber Rose hakubaki nyuma nae alitokelezea na twit yake kuhusu furaha ya kumpata mtoto wao mpendwa "The Bash|"
Tuesday, February 19, 2013
Monday, February 18, 2013
Click Hapo chini uangalie moja kwa moja kupitia hizo link hapo
LINK-01: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 |
LINK-02: MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2012 |
|
Matokeo ya kidato cha Nne 2012
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza
rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
---------------
---------------
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
---------------------
---------------------
1.0 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1 Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1 Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa
(a) Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67. Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 456,137 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa hawakufanya mtihani.
(b) Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,230 wakiwemo wasichana 182,978 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252 sawa na asilimia 55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.
(c) Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730 sawa na asilimia 11.23 hawakufanya mtihani.
4.0 MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a) Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.
(b) Watahiniwa wa Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 16,112 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 6,751 na wavulana ni 9,361.
5.0 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.
Idadi ya Wavulana
|
Idadi ya Wasichana
|
Jumla
|
|
I
|
1,073
|
568
|
1,641
|
II
|
4,456
|
1,997
|
6,453
|
III
|
10,813
|
4,613
|
15,426
|
I-III
|
16,342
|
7,178
|
23,520
|
IV
|
64,344
|
38,983
|
103,327
|
0
|
120,664
|
120,239
|
240,903
|
6.0 SHULE ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
------------
Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :------------
Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
ST. FRANCIS GIRLS
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS S.S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS S.S
|
69
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS S.S
|
88
|
PWANI
|
5
|
ROSMINI S S
|
78
|
TANGA
|
6
|
CANOSSA S.S
|
66
|
DAR ES SALAAM
|
7
|
JUDE MOSHONO S S
|
51
|
ARUSHA
|
8
|
ST. MARY’S MAZINDE JUU
|
83
|
TANGA
|
9
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
10
|
KIFUNGILO GIRLS S S
|
86
|
TANGA
|
11
|
FEZA GIRLS
|
49
|
DAR ES SALAAM
|
12
|
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
|
124
|
KILIMANJARO
|
13
|
DON BOSCO SEMINARY SS
|
43
|
IRINGA
|
14
|
ST.JOSEPH MILLENIUM
|
133
|
DAR ES SALAAM
|
15
|
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
|
64
|
KIGOMA
|
16
|
ST.JAMES SEMINARY SS
|
44
|
KILIMANJARO
|
17
|
MZUMBE SS
|
104
|
MOROGORO
|
18
|
KIBAHA SS
|
108
|
PWANI
|
19
|
NYEGEZI SEMINARY SS
|
68
|
MWANZA
|
20
|
TENGERU BOYS SS
|
76
|
ARUSHA
|
7.0 SHULE KUMI AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU ZAIDI
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI S.S
|
40
|
LINDI
|
2
|
NDAME S.S
|
41
|
UNGUJA
|
3
|
MAMNDIMKONGO S.S
|
63
|
PWANI
|
4
|
CHITEKETE S.S
|
57
|
MTWARA
|
5
|
MAENDELEO S.S
|
103
|
DAR ES SALAAM
|
6
|
KWAMNDOLWA S.S
|
89
|
TANGA
|
7
|
UNGULU S.S
|
62
|
MOROGORO
|
8
|
KIKALE S.S
|
60
|
PWANI
|
9
|
NKUMBA S.S
|
152
|
TANGA
|
10
|
TONGONI S.S
|
56
|
TANGA
|
8.0 TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1 Tathmini
ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule
mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo
zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na
vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini
ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i)
Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi
na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii) Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2 Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:
(i) Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao
wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya
walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii)
Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na
kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.
(iii) Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50
ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na
kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine
muhimu kitaaluma.
(iv) Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.
(v)
Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na
kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa
ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.
9.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a) Watahiniwa 28,582 wa
Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada wanayodaiwa
pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
(b) Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71
waliofanya Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya
Mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo
katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
10.0 MATOKEO YA MITIHANI YALIYOFUTWA
10.1 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao, watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.
Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama ifuatavyo:
S/N
|
AINA YA UDANGANYIFU
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
(i)
|
Watahiniwa
kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko
tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
|
04
|
(ii)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na ‘notes.’
|
170
|
(iii)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
|
590
|
(iv)
|
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani ‘impersonation”.
|
04
|
(v)
|
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
|
06
|
(vi)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
|
15
|
JUMLA
|
789
|
10.2 Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika Matusi Katika Skripti Zao
-----------
-----------
(i) Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“Written
responses to any examination question which carry words, drawings or
pictures connected to sex or abusive language in such a way that it
becomes offensive shall consitute an examination offence and a candidate
who commits such an offence shall be punished by the Council.”
Kutokana na kosa hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za Mitihani kinachosomeka:
“A candidate found to have committed an examination offence shall – (a) have his examination results nullified”
(ii)
Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti)
kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza
kuwavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali
itaangalia hatua zaidi za kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote
walioandika matusi.
Kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b)
cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote waliobainika kufanya
udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika skripti zao
hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani la
Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja (01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0 KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA CSEE na QT, 2012
(a) Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
· www.udsm.edu.ac.tz, au
(b) Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311. Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
18 Februari 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)