Kanisa katoliki laruhusu tembe za kuzuia mimba
Kanisa Katoliki nchini Ujerumani
limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya kuzuia mimba mara
tu baada ya kubakwa.
Tembe za kuzuia mimba
Uamuzi huu umefanywa kufuatia mkutano wa
viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja
aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili
mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema
kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.
Maaskofu nchini Ujerumani wamekuwa
wakijikuta njia panda, ambapo upande mmoja wanahangaishwa na msimamo wa
Kanisa Katoliki, na kwa upande mwingine tatizo lililompata mwanamke huyo
aliyebakwa, kufukuzwa na hospitali zinazosimamiwa na Kanisa hilo
zilizoko mjini Cologne.
Mwishowe Maaskofu hao walikubaliana kuwa itakuwa
halali ikiwa tembe hizo zitatumiwa na mwanamke aliyebakwa kwa lengo la
kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimba
Hii ina maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama
kifaa cha kuzuia kushika mimba lakini sio kuavya. Tembe hizo hutumiwa na
wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya tendo la ndoa.
Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, ambako Papa wa sasa alitoka, limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.
Ubishi kama huo nchini Marekani haukufikia
uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa zikibishania dawa hiyo kusema kuwa
ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha ndoa asubuhi inayofuata
mwanamke ameshika mimba au la.
No comments:
Post a Comment