Saturday, March 16, 2013

PAPA akutana na waandishi wa habari


PAPA akutana na waandishi wa habari

Papa Francis aliyechaguliwa hivi karibuni, amekutana na waandishi wa habari mjini Rome akisema kuwa atapenda kanisa maskini lenye lengo la kuwasaidia maskini.
Papa Francis akikutana na waandishi wa habari mjini Rome
Katika hatua ambayo Vatikani imesema inaonesha uwazi zaidi, Papa mpya alizungumza na mamia ya waandishi wa habari na alisema alichagua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi kwa sababu alikuwa mtakatifu wa amani, matumizi haba na kutumikia maskini
"Wakati wa uchaguzi wa papa mpya kando yangu alikuwa Askofu wa Sao Paulo, Claudio Hummes.
Ukweli ulipokuwa unakaraibia alinipoza.
Na kura zilipotimia thuluthi mbili alinikumbatia na kunibusu.
Aliniambia "usiwasahau masikini".
Na hilo limebaki nami...masikini, masikini"

No comments:

widgets

SPORTS NEWS