Tuesday, March 12, 2013

Bunge limeingia katika mzozo mwingine na Chadema


Naibu Spika, Job Ndugai 

Dar es Salaam. Bunge limeingia katika mzozo mwingine na Chadema baada ya kudaiwa kutoa ripoti polisi likitaka wabunge 28 wa upinzani waitwe ili wahojiwe katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na fujo zilizotokea bungeni Februari, mwaka huu.

Hata hivyo, chama hicho kikuu cha upinzani kupitia kwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, kimepinga hatua hiyo kikisema kamati hiyo haipo kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya 113(7) kwa kuwa imemaliza muda wake tangu Februari 8, mwaka huu na Spika hajaunda nyingine.

Hata hivyo, madai hayo ya Lissu yamepingwa vikali na Naibu Spika, Job Ndugai ambaye amesema kamati hiyo pamoja na nyingine mbili za Uongozi na ile ya Kanuni zinatambulika mpaka zitakapoundwa nyingine... “Hizo tatu ni ‘ongoing’ (zinaendelea) zisipokuwapo, basi Bunge hakuna.”

Mvutano huo ni wa pili katika siku za karibuni baada ya ule uliotokea katika Kikao cha Bunge la Februari baada ya Wabunge wa Chadema kuzua tafrani zilizosababisha kukatishwa kwa kikao kimoja cha Bunge hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Lissu alisema yeye na wabunge wenzake wapatao 28 watafika mbele ya kamati hiyo lakini wamekubaliana kuwa hawako tayari kuhojiwa nayo.
Mbali ya Lissu, jana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma alisema wabunge wa chama chake hawatakwenda kuhojiwa na kamati hiyo.

Lissu alisema njia iliyotumika kuwaita mbele ya kamati hiyo kwa kupitia polisi ni kinyume na utaratibu.
“Utaratibu uliotumika ni haramu kwa kuwa polisi ndiyo wametumika kutujulisha kwamba tunatakiwa tufike mbele ya kamati hiyo, kutumiwa ujumbe wa polisi si sawa kwani utaratibu wa Bunge unajulikana,” Lissu alisema na kuongeza:

“Kamati iliposema bungeni kuwa mimi na wenzangu watatu ni vinara wa fujo ilituhukumu tayari, hivyo kisheria wale wengine waliobaki walikuwa hawana makosa kwa mujibu wa sheria zetu.”

Ilidaiwa kwamba Ofisi ya Bunge iliiandikia Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kutaka kuwaelekeza makamanda wake kufikisha taarifa hizo.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema hakuwa na taarifa hizo na kuahidi kufuatilia.

Alipoulizwa kuhusu wabunge hao kuitwa kwa kutumia polisi, Ndugai alisema hakuwa na taarifa hiyo na kuelezea wasiwasi kwamba suala hilo limefikia hatua hiyo.
“Sidhani kama imefikia huko (kutumia polisi kuwaita wabunge), kwani kamati ina utaratibu wake wa kumwita mtu yeyote hata asipokuwa mbunge, kwa kweli sijui na sifikirii kama watakuwa wamefikia huko,”alisema Ndugai.

Mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kumpigia simu Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kumpa wito wa kufika mbele ya kamati hiyo ya Bunge na pia alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karatu (OCD), kuwapa taarifa Mbunge wa Karatu, Israel Natse na Mbunge wa Viti Maalumu Cecilia Paresso.


MWANANCHI

Saturday, March 9, 2013

CORD YAHIMIZA KUKUTANA NA HASSAN KABLA YA TANGAZO KUU



VIONGOZI wa muungano wa Cord wanataka waruhusiwe kukutana na mwenykiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kabla matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais kutangazwa.
Katibu Mkuu wa ODM, Profesa Anyang' Nyong'o amesema wametamaushwa na jinsi tume hiyo ilivyokiuka makubaliano yao kuruhusu maajenti wa vyama kuchunguza stakabadhi za hesabu ya kura kala kujumuishwa kwenye matokeo ya mwisho.
"Kilichotukasirisha ni jinsi IEBC livyoenda kinyume na maelewano tulioweka nao kuwa tungechunguza matokeo kabla yatangazwe, amesemma.
Kulingana nao, kura 17,000 kutoka maeneo bunge 120 hayakujumuishwa kwenye matokeo ambayo yanasubiriwa kutangazwa wakati wowote sasa.
Naibu Spika anayeondoka Farah Maalim amesema uchunguzi umeonyesha kura 170,000 zilizoeleweka katika maeneo bunge 20.
Mwenyekiti wa IEBC Issack Hassan amekuwa kwenye mkutano tangu asubuhi, na tangazo lililotarajiwa saa tano asubuhi litatolewa baada ya mkutano huo kukamilika.
Haijabainika kinachojadiliwa kwenye mkutano huo.



Tundu Lissu atunukiwa Nishani ya Heshima Marekani

Na Lissu,

"Wanabidii wenzangu, 

Nadhani sitakosea kuwashirikisha habari njema kidogo. Leo hii tarehe 6 Mei 2011, Chuo Kikuu cha Bridgeport kilichopo mji wa Bridgeport, Jimbo la Connecticut nchini Marekani kimenitunuku nishani ya 'Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Bridgeport' (Honorary Fellow of the International College). 

Citation ya nishani hii inasomeka kwamba 'Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu cheo cha Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa kwa kutambua utumishi wake uliotukuka katika kuendeleza haki za binadamu, ujenzi wa demokrasia na ulinzi wa mazingira katika Tanzania na Afrika...

' Kwa Kiingereza: 'In recognition of his inspired service for the furtherance of human rights, democratic institutions and the protection of the environment in Tanzania and in Africa..." 

Tuzo hii imekabidhiwa kwangu na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa Dr. Thomas J. Ward na Rais wa Chuo Kikuu cha Bridgeport Dr. Neil Albert Salonen. 

Kwa wale wote ambao wanaweza kuwa wanajiuliza kwa nini sijaonekana Mbeya na Nyanda za Juu Kusini, hii ndio sababu ya utoro wangu. 

Nitajiunga na makamanda wenzangu kuanzia wiki ijayo. 

Wasalaam, 

Tundu"

Nimetundika hiyo msg ya Mh. Tundu Lisu iliyoko "wanabidii" kwa kufurahishwa na kutambuliwa kwake kimataifaa na kujibu tashwishwi za kutokuwepo kwake kwenye maandamano ya Mbeya. 

Hongera Tundu Lisu, Hongera Chadema thamani yenu inaheshimika. 

Kitaeleweka tu.

FBI: Uamsho wana silaha za maangamizi

Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar, Musa Ali Musa alithibitisha kwamba jeshi lake limekuwa likishirikiana na FBI katika upelelezi na kwamba idadi ya waliokamatwa imeongezeka.

Ni kweli tumekuwa tukishirikiana na FBI katika upelelezi ilikuhakikisha wahusika wa tukio la kuuawa kwa Padri Mushi wanakamatwa .
Hii itasaidia kupunguza vitendo vinavyohusishwa na matukio ya kigaidi yakiwamo mauaji, alisema Kamishna Musa.
FBI wamekuja na orodha yao na polisi wetu wanafanya kutumwa “tukamatie yule na yule na yule” hawa waliokuja ni watu wasiyeamini mtu yeyote. Hawa ndio wale waliosema kwa kujiamini na jeuri kuwa Iraq kuna silaha za maangamizi, lakini baada ya walilokusudia kufanikiwa kwa maana kuwa baada ya kuvamia nchi ya watu na kuuwa mamilioni yawatu na kufanya uharibifu na ufisadi wa kutisha, wenyewe hao hao bila ya aibu wakasema kuwa Saddam hakuwa na silaha za maangamizi.

Kama alivyosema Rais wetu Mh Jakaya Mrisho Kikwete na kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Emmanuel Nchimbi na pia baadhi ya makamanda wetu wa Polisi, inavyoonekana tunawaamini sana ‘washirika’ wetu hawa. 
Lakini swali ni je, kama watatuambia uamsho wana kiwanda cha silaha za maangamizi kama walivyodai kuwa zipo kule Iraq tutaamini maadhali wamesema wao?
Tuna ubavu wa kupinga watakayosema kama tutakuwa na wasiwasi kuwa wanaongopa au sio sahihi? Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla ilisema Iraq hakuna silaha za maangamizi na ikapinga nchi hiyo,

Watu hawa alipokuja Bill Clinton hapa hawakuwaamini kabisa wana usalama wetu kiasi cha kumdhalilisha aliyekuwa Rais wetu Benjamin William Mkapa kwa kulinusisha gari lake kwa mbwa au tumesahau? 

Alipokuja ‘MzeeMzima’ George W Bush wakaweka vijana wao mpaka kwenye dari ya Ikulu yetu! Hivi sisi ndio tuliowaomba wapande au walipanda wenyewe bila hata yakungoja ruhusa yetu.

Mtu anakuja nyumbani kwako halafu anakupekuwa mpaka chumbani kwako. 
Yamewahi kufanyika mauwaji mengi sana nchini hapa, yakiwemo ya kamanda wa polisi Mwanza, lakini yote yalichukuliwa kama matukio ya kihalifu na vyombo vyetu vya usalama na sheria vikayashughulikia kwa umakini mkubwa.

IMETOKA taarifa yaJeshi la Polisi kuwa tayari maafande wetu wanashirikiana na makachero wa FBI kuwanasa watuhumiwa wa mauaji ya Padre Evarist Mushi.

The World's Third Laziest Country is 'Saudi Arabia ' '

Saudis are the third laziest people in the world after those of Malta in the Mediterranean Sea and Swaziland in Africa because of the high obesity rate in the Gulf Kingdom, a local newspaper reported on Sunday.

Around 40 per cent of Saudis are suffering from obesity but the rate is far less in the southern region of the Kingdom because of its rugged mountainous areas.

“In terms of laziness, the people of Saudi Arabia are ranked third in the world after the people of Malta and Swaziland,” the Saudi Arabic language daily Kabar said, citing a study by Dr Waleed Al Bakr, a well known endocrinology specialist.

He said obesity kills an average 20,000 people in Saudi Arabia every year, adding that women in the Kingdom are more vulnerable to obesity due to lack of exercise.

Saudi Arabia, the world’s dominant oil exporter and largest Arab economy, has a population of around 28 million, including nearly eight million expatriates. The country has one of the highest per capita incomes in the Middle East due its massive crude sales, standing at around $24,900 in 2012.
Saudis are world’s third laziest people: report - Emirates 24/7

Matukio baada ya kutangazwa mshindi Kenya

12:39 Lori lililokuwa limewabeba wafuasi wa Uhuru Kenyatta kutoka ngome yake ye Nyeri hususan eneo la Tetu, limeanguka, watu kumi wamejeruhiwa vibaya, mmoja amefariki na wengine zaidi ya 21 wanaendelea kupata matibabu

Wafuasi wa Uhuru Kenyatta

12:35 Maelfu ya wafuasi wa Kenyatta wakusanyika katika makao makuu yamuungano wa Jubilee, kumsubiri kiongozi wao wakati ukumbi wa Bomas ukiwa tayari kwa tangazo ya mshidni wa uchaguzi wa urais

11:32 Tume ya uchaguzi Kenya inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa kutangaza rasmi matokeo ya kura za urais

11:31 Mwandishi wa BBC Karen Allen kupitia twitter anasema moja ya kauli aliyoisikia leo ambayo imemfurahisha sana ni kumsikia mtu akisema kuwa wakenya ndio wameshinda uchaguzi kwa sababu wana taasisi mpya


09:51 Mjini Eldoret moja ya vitovu vya ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007, leo ni uwanja wa sherehe za ushindi wa Uhuru Kenyatta. Bendera na kila aina ya mabango zinazobebwa na wafuasi wa Kenyatta ni ishara ya furaha yao. Eldoret pia ni ngome ya mgombea mwenza wa Kenyatta, William Ruto

09:23 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu ambayo ndio ngome kuu ya Raila Odinga, Ann Mawathe anasema kuwa wafuasi wa Odinga wamenuna kwa kuwa mgombea wao ameshindwa kwenye uchaguzi lakini wanaendelea na shughuli zao kama kawaida
08:45 Mjini Nyeri moja ya ngome za Uhuru Kenyatta ni vifijo na nderemeo tupu barabarani kusherehekea ushindi wake


08:12 Mjini Nakuru mamia ya watu waliamka asubuhi na mapema kusherehekea barabarani kafuatia taarifa za mgombea wao wa urais Uhuru Kenyatta. Wameonekana wakibeba mabango na matawi kama ishara ya furaha yao
08:06 Josiah Mayaka Wa Kisii Kenya anasema kupitia Bofya facebook kuwa watu wengi Kisii wamesononeka sana ila kwa sababu limetendeka wamekubali matokeo shingo upande.
07:47 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameimba wimbo wa taifa wakiwa kando ya majengo ya bunge kusherehekea ushindi wa mgombea wao
Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto

07:39 Mjini Eldoret ngome ya William Ruto mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta sherehe zimeanza mapema na asubuhi baada ya matokeo kudhihirika wazi kuwa Uhuru Kenyatta ndiye mshindi07:35 Hanif Mohhamed wa Mombasa-Kenya kupitia ukurasa wa
Bofyafacebook naona mustakabali wa Kenya ni giza tupu, saa hii anasema anatafakari njia mubadala ya kukumbana na changa moto zitakazo wapata kama wakenya baada ya athari kuanza kuchimbuka.
07:26 Vifijo na nderemeo pamoja na milio ya honi katika barabara ya Kijabe mjini Nairobi kufuatia ushindi wa Uhuru Kenyatta 

07:08Alex Mulwa kupitia ukurasa wa Bofyafacebook anasema kuwa wakenya wamechagua viongozi ambao wataleta maendeleo na kuleta mabadiliko katika nchi yao. Alex ,kwa niaba ya wakenya anaomba ICC isitishe na kusimamisha kesi dhidi ya Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto ili kuwapa nafasi kuongoza bila wasiwasi

06:55 Wafuasi wa Uhuru Kenyatta wameanza kujitokeza katika baadhi ya sehemu za mji mkuu Nairobi kusherehekea ushindi wake

06:46 Uhuru Kenyatta ana kura 6,173,433 wakati Raila Odinga 5,340,54. Hii inampa Uhuru ushindi wa asilimia hamsini nukta tatu ambao unahitajika chini ya katiba mpya kwa mtu kushinda uchaguzi wa rais.
06:40 Tume ya uchaguzi baadaye leo itatangaza mshindi wa uchaguzi ingawa hesabu ya kura inaonyesha Uhuru Kenyatta anaongoza kinyang'anyiro.

Hesabu za kura 'zampa ushindi Kenyatta'


Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi. Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.

Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada yawakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.

    Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
    Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
    Waandishi wa BBC wanasema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
    Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi ya mshindi baadaye leo
    Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
    Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
    Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
    Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.

    Thursday, March 7, 2013

    HII NDIO KAULI YA SERIKALI KUHUSIANA NA TUKIO LA KUVAMIWA KWA MWANDISHI ABSALOM KIBANDA



    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi


    CORD wadai hujuma kwenye uchaguzi Kenya

    Mgombea mwenza wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna hujuma dhidi yao katika dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika ukumbi wa Bomas, na kwamba shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
    Hata hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
    Uhuru Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura 2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.Shughuli ya kuhesabu kura ingali inaendelea ingawa kwa mwendo wa kinyonga baada ya tume hiyo kutupilia mbali mitambo yake ya kuhesabu kura baada ya kugoma.

    Wananchi wa Venezuela waanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.


    Jeneza la aliyekuwa rais wa Venezuela  marehemu Hugo Chavez, limewekwa kwenye chuo cha kijeshi ambako litabakia kwa siku tatu ili kutoa fursa kwa waombolezaji kutoa heshima za mwisho. 
    Miongoni mwa walioshuhudia jeneza hilo likiingizwa katika eneo hilo ni mama mzazi wa Chavez, Bibi Elena, watoto wake watatu wa kike na mtoto mmoja wa kiume huku wengine waliokuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na Makamu wa Rais Nicolas Maduro na Rais wa Bolivia Evo Morales.
    Kutokana na kifo hicho, uchaguzi mpya wa nafasi ya rais utafanyika ndani ya siku 30.
    Aidha, upinzani nchini Venezuela umekubaliana kwamba kiongozi wa upinzani Henrique Capriles, agombee katika uchaguzi huo.
    Capriles alishindwa na Chavez katika uchaguzi wa urais uliofanyika miezi mitano iliyopita.

    Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!

    Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi. 

    Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

    Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?


    By Kibanda
    Quote"Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu 'kushuti' (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.

    “Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa..."

    Wednesday, March 6, 2013

    Venezuela’s President Hugo Chavez died four days ago

    The former Ambassador of Panama to the Organization of American States (OAS), Guillermo Cochez, said Venezuela’s President Hugo Chavez suffered brain death and who had died four days ago. According to statements given to international news channel NTN24, “the president suffered brain death since December 31 and have been disconnected from the machines that kept him alive for four days.”

    widgets

    SPORTS NEWS