"Wanabidii wenzangu,
Nadhani sitakosea kuwashirikisha habari njema kidogo. Leo hii tarehe 6 Mei 2011, Chuo Kikuu cha Bridgeport kilichopo mji wa Bridgeport, Jimbo la Connecticut nchini Marekani kimenitunuku nishani ya 'Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Bridgeport' (Honorary Fellow of the International College).
Citation ya nishani hii inasomeka kwamba 'Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu cheo cha Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa kwa kutambua utumishi wake uliotukuka katika kuendeleza haki za binadamu, ujenzi wa demokrasia na ulinzi wa mazingira katika Tanzania na Afrika...
' Kwa Kiingereza: 'In recognition of his inspired service for the furtherance of human rights, democratic institutions and the protection of the environment in Tanzania and in Africa..."
Tuzo hii imekabidhiwa kwangu na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa Dr. Thomas J. Ward na Rais wa Chuo Kikuu cha Bridgeport Dr. Neil Albert Salonen.
Kwa wale wote ambao wanaweza kuwa wanajiuliza kwa nini sijaonekana Mbeya na Nyanda za Juu Kusini, hii ndio sababu ya utoro wangu.
Nitajiunga na makamanda wenzangu kuanzia wiki ijayo.
Wasalaam,
Tundu"
Nimetundika hiyo msg ya Mh. Tundu Lisu iliyoko "wanabidii" kwa kufurahishwa na kutambuliwa kwake kimataifaa na kujibu tashwishwi za kutokuwepo kwake kwenye maandamano ya Mbeya.
Hongera Tundu Lisu, Hongera Chadema thamani yenu inaheshimika.
Kitaeleweka tu.
No comments:
Post a Comment