Saturday, March 9, 2013

CORD YAHIMIZA KUKUTANA NA HASSAN KABLA YA TANGAZO KUU



VIONGOZI wa muungano wa Cord wanataka waruhusiwe kukutana na mwenykiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kabla matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais kutangazwa.
Katibu Mkuu wa ODM, Profesa Anyang' Nyong'o amesema wametamaushwa na jinsi tume hiyo ilivyokiuka makubaliano yao kuruhusu maajenti wa vyama kuchunguza stakabadhi za hesabu ya kura kala kujumuishwa kwenye matokeo ya mwisho.
"Kilichotukasirisha ni jinsi IEBC livyoenda kinyume na maelewano tulioweka nao kuwa tungechunguza matokeo kabla yatangazwe, amesemma.
Kulingana nao, kura 17,000 kutoka maeneo bunge 120 hayakujumuishwa kwenye matokeo ambayo yanasubiriwa kutangazwa wakati wowote sasa.
Naibu Spika anayeondoka Farah Maalim amesema uchunguzi umeonyesha kura 170,000 zilizoeleweka katika maeneo bunge 20.
Mwenyekiti wa IEBC Issack Hassan amekuwa kwenye mkutano tangu asubuhi, na tangazo lililotarajiwa saa tano asubuhi litatolewa baada ya mkutano huo kukamilika.
Haijabainika kinachojadiliwa kwenye mkutano huo.



No comments:

widgets

SPORTS NEWS