Thursday, March 7, 2013

Wananchi wa Venezuela waanza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.


Jeneza la aliyekuwa rais wa Venezuela  marehemu Hugo Chavez, limewekwa kwenye chuo cha kijeshi ambako litabakia kwa siku tatu ili kutoa fursa kwa waombolezaji kutoa heshima za mwisho. 
Miongoni mwa walioshuhudia jeneza hilo likiingizwa katika eneo hilo ni mama mzazi wa Chavez, Bibi Elena, watoto wake watatu wa kike na mtoto mmoja wa kiume huku wengine waliokuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na Makamu wa Rais Nicolas Maduro na Rais wa Bolivia Evo Morales.
Kutokana na kifo hicho, uchaguzi mpya wa nafasi ya rais utafanyika ndani ya siku 30.
Aidha, upinzani nchini Venezuela umekubaliana kwamba kiongozi wa upinzani Henrique Capriles, agombee katika uchaguzi huo.
Capriles alishindwa na Chavez katika uchaguzi wa urais uliofanyika miezi mitano iliyopita.

No comments:

widgets

SPORTS NEWS