Thursday, March 7, 2013

CORD wadai hujuma kwenye uchaguzi Kenya

Mgombea mwenza wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna hujuma dhidi yao katika dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika ukumbi wa Bomas, na kwamba shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
Hata hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
Uhuru Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura 2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.Shughuli ya kuhesabu kura ingali inaendelea ingawa kwa mwendo wa kinyonga baada ya tume hiyo kutupilia mbali mitambo yake ya kuhesabu kura baada ya kugoma.

Taharuki imetanda na kuna hali ya wasiwasi kwani tume ya uchaguzi haijatangaza matokeo ya urais zaidi ya masaa arobaini na nane tangu wakenya kupiga kura.
Muungano wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua za kuchukua baada ya kudai hujuma katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu.
Hatua hii imelazimu tume hiyo kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa sasa
Musyoka vile vile amesema kuwa muungano huo una tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo wakisema sio ya kweli kwa kuwa hayawiani na yale waliyoyaleta maajenti wao.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na pia kuanza upya kwa shughuli ya kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani.
Musyoka alisema kuwa tume ya uchaguzi inastahili kutumia mitambo ya elektroniki kuhesabu kura kama inavyoagiza katiba ya nnchi, huku akiongeza kuwa muungano huo ungali unatafakari hatua za kuchukua ingawa kwa kufuata sheria.
Moja ya hatua inazotafakari kuchukua ni kwenda mahakamani kuitaka mahakama kusimamisha shughuli ya kuhesabu kura na kuanza tena

No comments:

widgets

SPORTS NEWS