Saturday, March 9, 2013

FBI: Uamsho wana silaha za maangamizi

Kamishna wa Jeshi la polisi Zanzibar, Musa Ali Musa alithibitisha kwamba jeshi lake limekuwa likishirikiana na FBI katika upelelezi na kwamba idadi ya waliokamatwa imeongezeka.

Ni kweli tumekuwa tukishirikiana na FBI katika upelelezi ilikuhakikisha wahusika wa tukio la kuuawa kwa Padri Mushi wanakamatwa .
Hii itasaidia kupunguza vitendo vinavyohusishwa na matukio ya kigaidi yakiwamo mauaji, alisema Kamishna Musa.
FBI wamekuja na orodha yao na polisi wetu wanafanya kutumwa “tukamatie yule na yule na yule” hawa waliokuja ni watu wasiyeamini mtu yeyote. Hawa ndio wale waliosema kwa kujiamini na jeuri kuwa Iraq kuna silaha za maangamizi, lakini baada ya walilokusudia kufanikiwa kwa maana kuwa baada ya kuvamia nchi ya watu na kuuwa mamilioni yawatu na kufanya uharibifu na ufisadi wa kutisha, wenyewe hao hao bila ya aibu wakasema kuwa Saddam hakuwa na silaha za maangamizi.

Kama alivyosema Rais wetu Mh Jakaya Mrisho Kikwete na kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Emmanuel Nchimbi na pia baadhi ya makamanda wetu wa Polisi, inavyoonekana tunawaamini sana ‘washirika’ wetu hawa. 
Lakini swali ni je, kama watatuambia uamsho wana kiwanda cha silaha za maangamizi kama walivyodai kuwa zipo kule Iraq tutaamini maadhali wamesema wao?
Tuna ubavu wa kupinga watakayosema kama tutakuwa na wasiwasi kuwa wanaongopa au sio sahihi? Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla ilisema Iraq hakuna silaha za maangamizi na ikapinga nchi hiyo,

Watu hawa alipokuja Bill Clinton hapa hawakuwaamini kabisa wana usalama wetu kiasi cha kumdhalilisha aliyekuwa Rais wetu Benjamin William Mkapa kwa kulinusisha gari lake kwa mbwa au tumesahau? 

Alipokuja ‘MzeeMzima’ George W Bush wakaweka vijana wao mpaka kwenye dari ya Ikulu yetu! Hivi sisi ndio tuliowaomba wapande au walipanda wenyewe bila hata yakungoja ruhusa yetu.

Mtu anakuja nyumbani kwako halafu anakupekuwa mpaka chumbani kwako. 
Yamewahi kufanyika mauwaji mengi sana nchini hapa, yakiwemo ya kamanda wa polisi Mwanza, lakini yote yalichukuliwa kama matukio ya kihalifu na vyombo vyetu vya usalama na sheria vikayashughulikia kwa umakini mkubwa.

IMETOKA taarifa yaJeshi la Polisi kuwa tayari maafande wetu wanashirikiana na makachero wa FBI kuwanasa watuhumiwa wa mauaji ya Padre Evarist Mushi.

No comments:

widgets

SPORTS NEWS