Thursday, March 7, 2013

Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi. 

Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

Kwahiyo kutekwa na kushambuliwa si uhalifu? Nani anaweza kumwamini Kova aliyewahi 'kuwasha' sinema ya Dr.Ulimboka na anayeshindwa kuizima hadi sasa?


By Kibanda
Quote"Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu 'kushuti' (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.

“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa..."

No comments:

widgets

SPORTS NEWS